March 11 2017, Naibu Spika wa Bunge la Tanzani Dr. Tulia Ackson aliongozana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kufanya ziara katika shule ya Sekondari Loleza iliyopo mkoani Mbeya ambayo aliwahi kusoma.
Dr. Tulia alizikuta baadhi ya changamoto zilizopo shuleni hapo ikiwemo ubovu wa vyoo na mabweni na akaahidi kuzitatua.
Lakini Dr. Tulia hakuishia hapo.. Alifunga safari hadi Hospitali ya Wilaya ya Tukuyu kujionea changamoto zilizopo na akaamua kutoa misaada mbalimbali katika hospitali za Wilaya ya Rungwe ikiwemo mashine ya kukaushia mionzi.
Full video nimekusogezea hapa chini….
VIDEO: Dr. Tulia na Waziri Nape kwenye Tulia Marathon Mbeya
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo