Mtanzania ambaye ni Miss Universe 2010, Hellen Dause alitajwa na jarida la Forbes Afrika kuwa miongoni mwa wajasiriamali walio chini ya umri wa miaka 30 kwa mwaka 2016 wanaotarajiwa kuwa mabilionea wajao.
Hellen Dause ni mwanzilishi wa kampuni iitwayo Nuya’s Essence ambapo ni kampuni inayohusika na kutengeneza bidhaa za asili kama vile vipodozi, sabuni n.k. Kwenye interview hii alipokutana na Millard Ayo ameeleza mambo aliyoyapitia kabla ya kuanzisha kampuni hiyo…..
>>>nilikuwa napenda sana kufanya biashara nilikuwa nataka niwe na kitu changu muda huo nilikuwa sijajua nataka kufanya biashara gani na muda huohuo nilikuwa nimejikita kwenye mambo ya unamitindo kwa hiyo nilikuwa napata matangazo ya TV kidogo na kazi ya kuonyesha mavazi na hii ndio ilikuwa inanipa hela ya pembeni nilipokuwa chuo nilipotoka pale nikashiriki Miss Universe‘
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA ALICHOSEMA HANSCANA KUHUSU KILE ALICHOKIFANYA ILI KUJULIKANA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE