Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Facebook
ZITTO KABWE
UAMUZI WA SERIKALI YA KENYA KUZUIA MAGARI YA KITALII YALIYOSAJILIWA TANZANIA KUINGIA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JOMO KENYATTA KWA AJILI YA KUCHUKUA NA KUSHUSHA WATALII
Tarehe 22 Desemba, 2014, Serikali ya Jamhuri ya Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kwenda kuchukua na kushusha watalii wanaotumia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Baada ya uamuzi huu wa Serikali ya Kenya, Waziri wa Maliasii na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu alifanya majadiliano na Waziri wa masuala ya utalii wa Serikali ya Kenya siku ya tarehe 16, Januari, 2015 ili kutafuta ufumbuzi wa kadhia hii. Matokeo ya mkutano wa Mawaziri hawa yalikuwa ni kusitishwa kwa muda katazo lililotolewa na Serikali ya Kenya kwa makubaliano kuwa yafanyike mazungumzo baina ya pande hizi mbili ndani ya kipindi cha wiki tatu kuanzia tarehe 16 Januari, 2015 ili kurekebisha Mkataba wa Ushirikiano katika sekta ya utalii wa mwaka 1985 kati ya nchi zetu mbili.
Kufuatia makubaliano hayo Wizara ya Maliasili na Utalii iliiomba Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki iandae kikao hicho cha pamoja katika muda uliopangwa. Kwa kuzingatia historia na uzito wa suala lenyewe, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki iliona umuhimu wa kuhusisha Wizara zingine husika za Uchukuzi, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira na Viongozi wa Sekta Binafsi ili kupata msimamo wa nchi wa pamoja kabla ya mkutano na Kenya.
Hivyo, vikao vya wataalam vimefanyika Dar es Salaam na Arusha hadi wiki ya kwanza ya mwezi huu wa pili kwa maandalizi ya kikao cha mwisho cha Mawaziri upande wa Tanzania kabla ya kukutana na wenzetu wa Kenya. Pamoja na kushauriana na Waziri mhusika wa Kenya (Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii, Bi. Phyllis Kandie) kusogeza mbele tarehe ya mkutano wa pamoja ili kuruhusu muda wa kutosha kwa majadiliano ya ndani na wadau, Bi. Kandie alimwandikia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Dkt. Richard Sezibera na kumnakili Waziri Nyalandu, kurejesha amri yake ya awali ambayo alisema inaendana na Sheria ya utalii na kanuni za uchukuzi za Kenya.
Serikali ya Tanzania kimsingi imesikitishwa na uamuzi huo wa Serikali ya Kenya kwani haujengi wala hauendani na dhamira njema ya Mkataba wa Kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuenzi njia ya mazungumzo, maelewano na maridhiano katika kufikia maamuzi. Suala la kurekebisha mkataba ulioingiwa na nchi hizi mbili kwa hiari miaka 30 iliyopita, si jepesi la kujadiliwa na Mawaziri wawili tu na kuwekeana ukomo wa muda katika kulipitia. Serikali ya Tanzania itaendelea na mchakato iliouanzisha wa kuhusisha wadau wote na kufikia uamuzi ambao itauwasilisha kwa Serikali ya Kenya kupitia vikao rasmi vya Jumuiya.
Pamoja na kwamba amri hii ya Serikali ya Kenya inaenda nje ya mkataba wa 1985 kwa kuvihusisha hata viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii, Serikali ya Tanzania itaheshimu na kuzingatia amri hiyo ili kulinda undugu na urafiki uliopo kati ya nchi zetu huku tukitafakari hatua za kuchukua ili kuondoa bughudha kubwa itakayotokea kwa watalii na wasafiri wetu wanaopitia uwanja huo wa Jomo Kenyatta. Aidha Tanzania itachukua hatua ya kuwafahamisha watalii na wageni wote wenye nia ya kutembelea vivutio vya kitalii vya Tanzania kutumia viwanja vingine vya ndege ili kuepuka kadhia na gharama zisizo za lazima.
Kwa upande wa Tanzania, viwanja vya ndege hasa vile vya Kimataifa vitaendelea kuwa sehemu ya malango ya kuingilia na kutokea kwenda kokote iwe ndani ya Jumuiya au nje ya Jumuiya na havitavichukuliwa kama vivutio vya utalii. Tanzania haitazuia magari ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au nchi nyingine yoyote kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua watalii wanaopitia katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao.
Mkataba wa mwaka 1985 kati ya Tanzania na Kenya ulilenga kutoa mwongozo wa ushirikiano katika Sekta ya Utalii kati ya nchi zetu mbili. Aidha, makubaliano hayo yalielekeza maeneo muafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii huku ikizingatiwa kuondoa bugudha kwa watalii. Maeneo hayo ni pamoja na miji ya mipakani pamoja na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili ikiwemo Nairobi ambako kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Jomo Kenyatta kipo.
Blog
Jiachie Blog
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumbai iliopo mtaa wa Libya na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kilkuwepo eneo la tukio lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo huku kikosi cha zimamoto na magari nayo yaliendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Michuzi
MELI KUBWA YENYE UREFU WA MITA 244 YATIA NANGA BANDARI YA DAR
Meli kubwa MSC Martina yenye urefu wa mita 244 na upana wa mita 32.2 ikiwa na uwezo wa kubeba makontena 2,411 imefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mhandisi Madeni Kipande amesema, mafanikio hayo ni juhudi zilizofanywa na Mamlaka kuzitangaza bandari zake pamoja na uboreshwaji wa huduma.
“Ujio huu wa meli kubwa za mizigo kama hizi ni faraja kubwa sana kwetu kwani pia utaongeza uingiaji wa mizigo kwa wingi na hatimaye kuleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho,” alisema Mhandisi Kipande. MSC Martina Kampuni ya Mediterranean Shipping Company (MSC) ni miongoni mwa meli kubwa na za kisasa ambazo zimefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kupakia na kupakua mzigo.
Rweyunga
WAHAMIAJI HARAMU 27 WAFA KWA BARIDI WAKIWA BAHARINI NCHINI ITALIA
Wahamiaji haramu wapatao 27 wamekufa kutokana na baridi kali baada ya kuokolewa karibu na kisiwa cha Lampedusa, walinzi wa Pwani ya Italia wameeleza.
Wahamiaji hao ni sehemu ya kundi la wahamiaji 105, waliokutwa wakielea baharini kwenye boti ya kujaza upepo, Kilomita 160 kutoka kwenye eneo la Italia.
Wahamiaji hao waliomba msaada kupitia simu ya mfumo wa setilaiti, baada ya kupata matatizo, wakati mawimbi ya bahari yakiwa na ukubwa wa mita nane, huku hali ya hewa ikiwa inaelekea kuganda.
BBC: Ngasa aomba Yanga imlipie deni
Mshambuliaji machachari wa klabu ya Yanga, ameiomba klabu yake kumlipia deni analodaiwa benki ili aweze kucheza kwa bidii na kuwa mfungaji bora.
Ngasa aliamriwa kulipa deni la Sh 45 milioni kwa kosa la kujiunga na Yanga bila kufuata utaratibu akitokea Simba, hivyo , kwa makubaliano, analazimika kukatwa Sh500,000 (wastani wa dola 280) kila mwezi kutoka katika sehemu ya mshahara wake anaoupata kutoka Yanga ili kulipa deni.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro, benki , baada ya kukata 500,000, ililazimika kuchukua mshahara wote wa Ngasa katika miezi ya hivi karibuni ili kufidia deni analodaiwa baada ya uongozi uliopita wa klabu hiyo kushindwa kupitisha benki mshahara wake benki kwa muda unaokisiwa mwaka mmoja, hivyo kutolipa kwa mujibu wa makubaliano na benki kulazimika kumuacha mchezaji huyo bila senti.
Ngasa aliripotiwa kusema kuwa hali yake ya kifedha “financial status” ni mbaya na kushindwa kucheza vizuri, na kuiomba Yanga kuangalia namna ya kumsaidia kulipa ili aweze kubakiwa na fedha za kutoka.
“Tutakaa na Ngasa tuangalie namna ya kumsaidia”.
“Licha ya matatizo aliyonayo, ameonesha kuwa ni mchezaji anayejituma na magoli mawili aliyofunga hivi karibuni na kutupa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika ligi kuu inaonesha anavyoithamin i timu yake”, alisema Muro.
Tanzania yasaini hati ya makubaliano
Tanzania imetia saini rasmi Hati ya Makubaliano ya Mkutano wa mtoto wa kike uliofanyika mwaka jana nchini Uingereza.Kwa mujibu wa waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wa Tanzania, Sophia Simba, kusaini kwa hati hiyo, ni kuonyesha dhamira ya serikali ya nchi hiyo katika kupambana na kuhakikisha inatokomeza vitendo vya ukeketaji na ndoa za utotoni.
Bongo Movie
Swebe: Sijaacha Kuigiza!!
Pamoja na kupata dili la kutangaza katika kituo cha radio mwigizaji mkongwe, Adam Melele “Swebe Satanta” amesema ajaacha uigizaji.
Swebe alisema kuwa bado anaigiza na nikiongozi wa kundi jipya lianalounganisha wakongwe katika tasnia ya filamu na maigizo la Kaone Sanaa linalorusha tamthiliya yake katika TV one.
‘Naingiza kama kawaida isipokuwa inategemea napata maslai kwa mtindo gani? Harafu pia unatakiwa ujue kama mimi ni kiongozi wa kundi la Kaone Sanaa, naigiza pia nikitangaza sifungwi nisiigize” swebe alisema.
Mwananchi: Dk Mwakyembe: Hatutazuia magari ya kitalii toka nchi jirani
Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Harison Mwakyembe amesema Tanzania haitazuia magari ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki au Nchi nyingine kuingia katika viwanja vyake vya ndege kuleta au kuchukua Watalii wanaopitia katika viwanja hivyo na kwenda katika nchi zao.
Akizungumza na waandishi wa hahabari jijini Dar es Salaam leo, Dk. Mwakyembe amesema serikali ya Kenya wameenda kinyume na mkataba wa mwaka 1985 kwa kuvihusisha viwanja vya ndege kuwa sehemu ya vivutio vya utalii jambo lililopelekea kukatazwa kwa magari ya Kitalii yaliyo sajiliwa Tanzania kuingia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata.
Mwanaspoti
MWIGIZAJI wa filamu na muziki Bongo, Frola Mvungi yupo katika wakati mgumu akihofia mtoto wake, Tanzanite Hamis Baba kutekwa na watu wasiojulikana.
Msanii huyo amedai kwamba kuna watu ambao wamefika nyumbani kwake zaidi ya mara tatu kumtaka mfanyakazi wa awape mtoto huyo.
“Nimepatwa na hofu sijui kama watu wanataka kuiba mtoto wangu ama vupi? Mara ya kwanza walikuja watu wawili, mwanamke na mwanaume wakamwambia dada wa kazi kuwa nimewaagiza wamchukue Tanzanite wampeleke shule, dada akawakatalia,” alisema Frola.
TZA: Video ya Diamond Platnumz yachezwa kama #SmashHit kwenye kituo kikubwa cha TV
Video ya Nitampata Wapi ya Diamond Platnumz baada ya kupitishwa kuchezwa kwenye kituo cha TV cha kimataifa cha Trace Urban cha Ufaransa, bado imeendelea kufanya vizuri mpaka kupewa nafasi ya kuchezwa kama SmashHit kwenye kituo hicho.
Baada ya muda Diamond akaandika kupitia ukurasa wake wa instagram na kuandikia ‘Ingefikia hapo bila nguvu na Support toka nyumbani… toka Moyoni mwangu, Nawashkuru sana….na Aminini kauli yangu “Ndio kwaanza nimeanza… Angalieni Snema Huu Mwaka