Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Ni wazi uwepo wako kama kiongozi unategemea ufadhili wa biashara ya madawa ya kulevya kama umeshindwa kukabiliana nayo katika nafasi yako.
— Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) February 2, 2015
Wananchi wanachagua viongozi ili watende. Tunapitia miaka 10 ya viongozi kulalamika, wakati mwingine hata kulia machozi badala ya kutenda.
— Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) February 2, 2015
TZS 1 trln imezuiliwa na wahisani. Nchi sasa inaishi kwa 800bn za TRA kwa mwezi. Rais bado anasafiri akitumia zaidi ya milioni 20 kila siku.
— Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) February 2, 2015
Unapong’oa fito zilizojenga nyumba ambamo ndugu mnaishi ni wazi kwamba tayari umejijengea mahala pengine pa kuishi endapo hapa pataanguka.
— Dr Wilbrod Slaa (@wilbrodslaa) February 2, 2015
Nitatoa Kitabu changu mwezi wa pili. Kinaelezea fikra mpya za Tanzania ya kizazi cha mabadiliko. Nimekiandika kwa muda mrefu kidogo.
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) February 2, 2015
Tunapoteza zaidi ya bilioni 4 kwenye foleni za mabasi Dar es salaam. Kwenye kitabu changu ninapendekeza a multi-modal city transit system
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) February 2, 2015
Kwenye kitabu changu, napendekeza tupunguze ukubwa wa serikali kwa kupunguza idadi ya mawizara, wakala za serikali na tume…
— Hamisi Kigwangalla (@hkigwangalla) February 2, 2015
Instagram
Tunda Man: Nitakuwa mchoyo wa fadhila nikishindwa kumshukuru sana @mkubwafella na @babutale kwakunifikisha mpaka hapa nilipo na bado wanaumia kwa ajili yangu…Kuunganisha TIP TOP na TMK familly.na kufanya kuwa makundi bora na yaliyodum mpaka sasa.thanx pia mwanangu @chambuso kwa mchango wako kwangu TIP TOP 4LIFE.
Kajala: Naomba niwaulize binadamu alie kwambia mm nikivaa hivi nitamualibu mtoto nani acheni akili za kijinga kwasababu wengi wetu tunajua kabisa mtoto awi na tabia mbaya kwasababu anamuona mama yake kavaa dira au tumbo wazi sisi zamani wazazi wetu walikuwa wanavaa hivi lakini mbona tuliwasumbua mnaboa na kukera pia kama mtoto wangu atahalibika kisa kaniona mimi nimevaa tumbo wazi utakuwa ni umbumbu wake na ujinga wake lakini sidhani kama mavazi yanamualibu mtoto nahisi nimalezi pekee yake kama nakuboa usipite hapa tafadhali.
Clouds FM: BASATA YAANZISHA MFUMO MPYA
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limeanzisha kanzidata ‘database’ ya kuhifadhi kumbukumbu na taarifa mbalimbali za kumbi za starehe na burudani nchini ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu sahihi katika sekta ya sanaa.
Akizungumza jijini hivi karibuni wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Basata kuhusu matumizi sahihi ya kanzidata, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mngereza alisema wanaimani malengo ya kuhifadhi taarifa na takwimu zote zihusuzo sekta ya sanaa yatatimia.
Blog
BBC Swahili
Rais wa Nigeria anusurika bomu
Bomu limelipuka kazkazini mwa Nigeria nje ya uwanja mmoja wa soka ambapo rais Goodluck Johnathan alikuwa amehutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuko huo ulitokea katika eneo moja la kuegesha magari dakika chache tu baada ya rais huyo kuondoka katika uwanja huo uliopo mji wa Gome.
Bwana Johnathan anafanya kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi unaotarajiwa tarehe 14 mwezi Februari,lakini anakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa kundi la Boko Haram huku kundi hilo likiimarisha mashambulizi yake.
Siku ya jumapili watu watano waliuawa na bomu huko Gombe.
Mwananchi
Kikwete: Mgombea urais bado hajajitokeza
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amedokeza kuwa atakayekuwa mgombea wake wa urais baadaye mwaka huu ni yule ambaye hajajitokeza mpaka sasa.
Akihutubia jana katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho mjini Songea, mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema: “Wapo watu wenye sifa zote za urais lakini hawajitokezi na hata wakiambiwa kuwa wanaweza husema hawajajiandaa. Hawa ndiyo tunaowahitaji kwa kuwa wanahitaji kukumbushwa tu.”
Ebola ‘yaua’ soko la utalii Arusha
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato), Willy Chambulo alisema hayo hivi karibuni na kuongeza kuwa hali hiyo imesababisha hoteli za kitalii na nyingine kupunguza wafanyakazi.
Chambulo aliiomba Serikali kusaidia sekta hiyo kwa kueleza kuwa ebola haijangia Tanzania ili kuondoa wasiwasi kwa baadhi ya watalii ili waendelee kuja nchini na kuongeza pato la Taifa.
“Hata hoteli zangu sita nimezifunga na wenzangu ambao hawajafunga nao watafunga tu, kwa sababu ya kukosa watalii wanaoogopa ebola ambayo kwetu haipo,” alisema Chambulo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ebola na tuhuma za ugaidi vimetikisa sekta ya utalii.
Alisema kila mwaka Tanzania imekuwa ikipokea watalii 250,000 wanaopitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Kenya, lakini hivi sasa idadi hiyo imepungua.
Waziri Nyalandu alisema mwaka 2015 umepokewa vibaya katika sekta ya utalii kutokana na sakata hilo.
Saleh Jembe
KOPUNOVIC AGOMA MATOLA KUONDOKA, AMSHAWIKI, AKUBALI KUBAKI
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amebadili uamuzi wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya bosi wake, Goran Kopunovic kusisitiza: “Haondoki mtu.”
Habari za uhakika kutoka Simba zimeeleza, Kopunovic aliutaka uongozi wa Simba kumuacha azungumze na Matola ambaye aliueleza uongozi wa klabu hiyo ameamua kuondoka katika timu kubwa.
“Kweli, kocha alisema asingependa kumuacha Matola ambaye amekuwa mchapakazi na mtu anayejua kuifanya kazi yake.
“Hivyo aliuomba uongozi azungumze na Matola halafu atawapa jibu, kweli alifanya hivyo na mwisho wakaelewana.
“Hata baadhi ya viongozi nao walimfuata Matola na kuzungumza naye kuhusiana na suala hilo na kumsihi abadili uamuzi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Nataka nikuhakikishia, Matola hana tatizo, hata wale mashabiki waliomzomea hawajui lolote. Viongozi wanaotaka maslahi ya Simba wanajua umuhimu wake na anavyojituma.”
Alipotafutwa mwenyewe Matola, alipokea simu na kusema: “Kwa sasa naomba mniache kidogo, nitalizungumzia vizuri siku nyingine.”
KOPUNOVIC ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE, ASISITIZA AVUMILIWE KIDOGO
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutulia na kuendelea kumuunga mkono katika kipindi hiki anachoendelea kukisuka kikosi chake ili kiweze kuendana na hadhi ya klabu hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1936.
Kocha huyo mwenye uraia wa Serbia alisema kuwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo waendelee kuwa watulivu na wavumilivu huku wakimuunga mkono katika harakati zake za kuhakikisha kikosi chake hicho kinakuwa sawa.
Bado naendelea kukisuka kikosi changu, hivyo mashabiki wetu wawe watulivu na waendelee kutuunga mkono ili tuweze kufikia malengo yetu tuliyojiwekea.
“Tangu nianze kuifundisha timu hii ndiyo kwanza kesho Jumatatu (leo) natimiza mwezi mmoja, hivyo ni muda mchache sana lakini nimekuwa nikijitahidi kuhakikisha tunakuwa vizuri,” alisema Kopunovic.
Michuzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Hamisi Hassan Mwinyimvua kuwa Naibu kuwa Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha
Kabla ya uteuzi wake Dkt Hamisi Hassan alikuwa msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa masuala ya uchumi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook