Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekagua magari ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yaliyoandaliwa kwa ajili ya kubeba korosho za wakulima endapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ifikapo Jumatatu tarehe 12 Novemba, 2018 saa 10:00 Jioni.
Mapema akitoa taarifa ya maandalizi ya kutekeleza jukumu hilo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen. Venance Mabeyo amesema JWTZ imetayarisha magari ya uwezo tofauti 75 yenye uwezo wa kubeba jumla ya tani 1,500 kwa mpigo na kwamba tani nyingine 500 zitabebwa na meli ya kijeshi (Landing Craft) ambayo inaweza kutia nanga mahali popote katika ufukwe wa bahari.
“Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu tupo tayari kutekeleza jukumu hili” amesema Jen. Mabeyo.
Rais Magufuli Jeshini leo “Lazima tujipange, JWTZ na JKT mfikirie, huu ni Utumwa”