Top Stories

RPC mpya wa Mbeya kaamkia Stendi ya mabasi kakutana na haya

on

Siku chache baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Saimoni Sirro kufanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi kwa baadhi ya Mikoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Urich Matei ameanza kazi kwa kukagua magari ya abiria yaendayo mikoani na kuwapima ulevi madereva.

Aidha katika zoezi hilo la ukaguzi mabasi mawili yamebainika kuwa na hitilafu za kiufundi hivyo kuwekewa zuio la kusafirisha abiria hadi pale yatakapofanyiwa marekebisho.

Akizungumzia baada ya zoezi la ukaguzi Kamanda Matei, amewataka madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu za usalama Barabarani.

Ameyataja magari ambayo yamebainika kuwa na hitilafu na kuwekewa zuio la kusafirisha abiria mpaka yatakapofanyiwa marekebisho kuwa ni Kampuni ya mabasi ya Premier yanayofanya safari zake Mbeya Kwenda Mwanza na Kampuni ya Network ambayo yanafanya safari zake Mbeya kwenda Sumbawanga.

Akizungumzia kuhusu mkakati wa Jeshi la Polisi wa kukomesha vitendo vya uhalifu Mkoa wa Mbeya, Kamanda amewataka wananchi kutoa taarifa sahihi za wahalifu kwani wa ndio wapo karibu na jamii.

“Afadhali ulime Bangi kuliko Kahawa” wananchi wamemwambia Prof. Tibaijuka

Soma na hizi

Tupia Comments