Nafahamu tumezoea usafiri wa mabasi au magari tukiwa ndani ya miji ili kwenda sehemu tofauti leo imenifikia hii ya kijiji cha Giethoorn nchini Netherlands ambapo barabara zao ni maji na boti ndio zinatumika kama usafiri kuzunguka kijijini hapo.
Giethoorn ina wakazi 2,600 na madaraja yapo 180 ambayo ndio kama vituo watu wanaposhuka na kuingia majumbani mwao na pia kutembeleana, kwenda sokoni na sehemu zote unazozifahamu kwa ajili ya maisha ya kila siku.
Nimekuweke picha za kijiji hicho ujionee mazingira yake na jinsi madaraja hayo yalivyotengenezwa kwa kila kituo.
VIDEO: Hali ilivyo stendi ya Ubungo DSM msimu wa sikukuu ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, Bonyeza Play hapa chini kutazama
Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE