Waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa mpaka wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya za Kiteto na Kilindi ukiwa ni mgogoro uliochukua muda mrefu na kuanza kusuluishwa toka mwaka 1997.
Suluhu imepatikana kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri mkuu na kuwakutanisha Wakuu wa sehemu hizo mbili wakiwemo pia Wabunge wa Kiteto na Kilindi, Wenyeviti wa Halmashauri na Madiwani.
Amesema nchi ilishaweka mipaka ya mikoa na wilaya tangu zamani na kumbukumbu zipo zikiwemo za mipaka hiyo tangu mwaka 1961 na hakuna mabadiliko ambapo Serikali kupitia Wizara ya ardhi itakwenda kuweka alama vizuri kwa kifaa maalum na viongozi wa Wilaya hizo watashirikishwa.
Unaweza kutazama kwenye hii video hapa chini kuona ilivyokua.