Baada ya taarifa ya Habari ITV utaona kuna Kibonzo ambacho huandaliwa na mchoraji Nathan Mpangala, huenda wengi hatufahamu kuhusu yeye.
Kapata nafasi kuonekana kwenye show ya MKASI March 02, ameanza kuzungumzia safari yake ilikoanzia mpaka kuingia kwenye uchoraji wa katuni; “Baada ya kumaliza masomo ya Sekondari nikaenda kusoma fine arts.. Baada ya kumaliza nikajikuta niko tu sielewi nakwenda wapi. Nikajikuta nimeanza tu kuchora katuni, nakumbuka mchoro wangu wa kwanza ilikuwa kwenye gazeti la Uhuru.. ilikuwa ni hadithi a michoro, ile michoro imeanza kutoka mimi sina habari“
Mother alivorudi nyumbani akaniambia mwanangu nimeambiwa ofisini kwamba jina lako limeonekana kwenye gazeti la Uhuru, nilikuwa kama nimezaliwa upya. Baadaye tukawa na Gazeti la Sanifu ikawa kama kijiji cha wachoraji.. wachoraji tukawa tunakutana wengi tunashare ideas..”
Tofauti ya katuni kwenye gazeti na katuni za kwenye TV; “Tofauti ya kuchora katuni kwenye gazeti kila siku na kuchora kwenye TV, kwenye gazeti naweza kuchora mchoro ambao ni fumbo sana lakini kwenye TV itabidi nichore message ambayo iko clear kwa sababu kuna sekunde kama 35 hivi.. kama nitakuwa nabanabana kama mafumbo tofauti na gazeti mtu asipoelewa sasa hivi atafika nyumbani atacheki kidogo..”
Ni kitu gani kigumu kwenye kazi yake?; “Katika vitu vinanipa shida bora unakuja na idea halafu mhariri anakwambia hebu tafuta nyingine.. Kuliko ile unafika asubuhi ‘Nathan hebu mchore fulani’, kuchora ni maoni binafsi..”
Sifa za mchora katuni; “Hizi katuni za maoni msingi mkubwa lazima uwe unafuatilia masuala ya kila siku..”
Hapa ametaja baadhi ya watu ambao ni rahisi kuchoreka; “Kama mtu anakuwa na features ambazo zinaonekana kirahisi ni rahisi kuchoreka, kwa mfano mwalimu Nyerere.. Mizengo Pinda.. Benjamin Mkapa..”
Kazi ya uchoraji na mazingira ya Uchaguzi mkuu 2015; “Kama wamiliki wa vyombo vya habari wataamua kutoka kwenye misingi na taratibu za undeshaji wa vyombo vya habari automatically wanakuja kuwaathiri wachoraji, maripota. Ilishasemwa kama wewe unamiliki vyombo vya habari ujiweke pembeni halafu utengeneze Management ikuendeshee biashara…”
Kuyasikiliza yote yako hapa, bonyeza play..
Jinsi alivyoingia ITV kuchora vibonzo vya taarifa ya Habari; “Nilikuwa na wazo hilo.. nilikuwa kwenye mkutano Arusha nikapata simu kutoka kwa Mkurugenzi wa ITV na Radio One, akasema ukirudi njoo tuonane.. Nilivofika tu nikatia timu. Akasema nenda kafikirie tunachotaka tuwe na katuni ambayo itakuwa inabeba ujumbe fulani kila siku ndio ilipoanzia kibonzo..”
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook