Jina lake linafanana na aliyekuwa Kocha wa Timu ya Tafa TZ, Marcio Maximo, yeye anaitwa Mecky Mexime, amesikika kwenye show ya Mkasi, katika aliyoyaongea kuna haya kumi kutoka kwake, safari yake kwenye soka, uchawi na soka, shule…
Hivi ndivyo safari yake kwenye soka ilivyoanza; “Tangu shuleni nilikuwa madarasa ya chini lakini timu ya shule nilikuwa nacheza.. Nikapata bahati ya kwenda Mtibwa, nilikuta watu kibao wako kwenye majaribio, lakini nilivyofika jioni, asubuhi nimeenda ofisini wakasema huyu tunamfahamu haina haja ya majaribio.. Asubuhi yake nikasaini fomu nikapewa chenji kidogo tu, sio kama sasa hivi watu wanapewa mahela makubwa“
Safari yake ya soka ilianzia Mtibwa kama mchezaji na ikaishia Mtibwa kama kocha; “Viongozi wa Simba au Yanga tumekuja hivi tunaongea bwana tunakutaka.. lakini kati yenu watatu mmoja ananipigia simu, ‘Mecky tumekaa kwenye mazungumzo lakini mi’ naona wewe bora ubaki Mtibwa usije huku”
Kingine ni hiki cha umuhimu wa Makocha kusomea mpira; “Kusoma ni muhimu zaidi kwa sababu unavyoenda kusoma unaambiwa mazoezi jinsi ya kufanya.. wachezaji afya zao.. muda wa kupumzika.. Kila hatua unayoenda na muda wa kupumzika either mrefu au mfupi..”
Nini kilimfanya amekuwa Kocha?; “Sikuwa na wazo la kuja kuwa mwalimu, Maximo ndio alionipa kipindi kile nacheza timu ya taifa nilikuwa namsaidia mambo mengi sana, alionna kipaji changu akanishauri akaniambia hapa bado unacheza zikitokea kozi nenda hata mimi naweza nikakusapoti. Nilipostaafu timu ya taifa lakini nikawa nacheza Mtibwa kozi zikatoka nikawa naenda lakini huku bado nacheza”
Ishu ya wachezaji wa TZ kuwa na majina ya wachezaji wa nje; “Haya majina mashabiki ndio wanatoa huwezi kukataa, wewe mwenyewe huwezi tu ukajipa tu kwa mfano Nadir Haroub Cannavaro..”
Nafasi ya makocha wazawa kwenye timu za TZ; “Makocha sisi wazawa kwanza sisi wenyewe tu hatuaminiani, halafu angalia nani anaeleta Kocha, ana taaluma ile ya mpira au kwa sababu mtu ana helka zake basi analeta Kocha.. Jana tu nimesoma gazeti ‘Matola afukuzwa Simba’, Simba wamefanikiwa kwa sababu wana vijana wengi na yeye ndio ambaye amewakuza, tunaenda Mapinduzi ‘Mzungu’ kaja sijui mechi tatu za mwisho sijui.. wakachukua Ubingwa lakini timu alikuwa nayo Matola. Angalia Mbeya City ilifanya vibaya watu wakaleta kelele lakini angalia sasa hivi Mbeya City iko wapi..”
Imani za kishirikina na soka; “Mi’ sizani Mtanzania atokeze hapa hana imani hizo.. zipo watu hela wanaliwa kutokana tu na imani..”
Ana hiki cha kusema kuhusu mpira wa TZ; “Inatakiwa tuimarishe ligi yetu, tuhakikishe wachezaji wanaperform kwenye ligi yetu Tanzania na isiwe ligi ya magumashi.. akina Samatta wanatakiwa wawe wengi hapo tunaweza tukapiga hatua“
Anauchukuliaje utendaji wa viongozi TFF; “Uongozi unajitahidi, siwezi kuzungumzia sana kwa sababu siko huko.. Mimi nimechezea timu ya Taifa zamani ilikuwa ina shida sana tunakaa Salvation army, mchezaji umelala juu wanapita wadudu wale nguchiro”
Hapa anataja kikosi ambacho anatamani angecheza nacho timu moja; “Namba moja anakaa Mwameja, mbili Kassim Issa.. tatu Alphonse Modest.. nne na tano walikuwepo akina George Masatu, Boniface Pawasa, Waziri Mahazi, Suleiman Matola.. sita Hussein Masha.. saba Steven Mapunda, nane Salvatory Edward, tisa Monja Liseki, (10) Amir Maftah, (11) Edibili Lunyamila“
Iko yote hapa kwenye hii sauti, Bonyeza pla kuisikiliza
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook