Baada ya kuwepo kwa mfululizo na mapokeo chanya kwa tamthiliya za kigeni nchini na kuingiziwa sauti na watanzania kufanya vizuri nchini, sasa ni zamu ya tamthiliya mpya ya kihindi inayoitwa Waaris ikiwa na maana Mrithi kuonesha Tanzania ikiwa imeletwa kwa lugha ya Kiswahili, tamthiliya hiyo inatajwa kuwa itafanya vizuri.
Miongoni mwa wasanii walioshiriki kuingiza sauti za Kiswahili katika tamthiliya ya Waaris ni Vyonne Cherry (Monalisa), Godliver Gordian, Sophie na Rakheem David ambao wana uwezo wa hali ya juu katika kuingiza sauti na kwa ujumla wameitendea haki Waaris, itakuwa inaoneshwa Alhamisi na Ijumaa, hii inaonekana msanii na muigizaji Monalisa anaendelea kuonesha umahiri wake katika kuzifanyia sauti tamthiliya za kigeni kiasi cha kuwa anaaminiwa zaidi.
“Tunaendelea kujipambanua kama wafalme wa Burudani za kifamilia, na tamthiliya hii mpya ni aina ya maudhui ambayo yanaweza kuangaliwa na familia nzima. Tamthiliya ya Waaris ama kwa Kiswahili Mrithi itaanza kuonekana kwenye chaneli yetu ya ST Swahili siku za Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 2:30 hadi saa 3:30 Usiku.”>>>David Malisa
MAAJABU: Siku nne Mtoto anatapika mawe, Bibi yake nae arushiwa mawe batini