Leo July 30, 2019 Mfanyabiashara Hamis Said (38), mkazi wa Geza Ulole Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya mauaji (mke wake), Naomi Marijani.
Said amesomewa kosa lake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.
Wakili Wankyo ameeleza mtuhumiwa ameshitakiwa kosa hilo kwa mujibu wa Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Katika kosa hilo, inadaiwa alilitenda Mei 15, 2019 katika oneo la Genzaulalo Kigamboni Dar es Salaam ambapo alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
Baada ya kusomewa kosa hilo mshitakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka.
Wakili Wankyo amedai kuwa Upelele wa kesi hiyo haujakamilika kwani unaendelea, hivyo anaomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Kesi imeahirishwa hadi August 13, 2019 mshitakiwa karudishwa rumande.
Inakumbukwa kuwa Hamis anadaiwa kumuua mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.
MBOWE AANGUSHA MAOMBI NA MAGUFULI, JPM KAFUNGUKIA “UWE MCHUNGAJI”