Vyama kumi na moja vya Siasa vimemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa kuitisha Mkutano wa Vyama vya Siasa haraka ili kujadili changamoto ambazo zinajitokeza katika mchakato wa kurudisha fomu na kupitidha Wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini unatarajiwa kufanyika mwezi huu.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Vyama hivyo Abdul Mloya ambavyo ni DP, SAU, NRA, ADC, UDP, UMD, CCK, TADEA, DEMOKRASIA MAKINI, TLP, AAFP akisema kuwa Wasimamizi wa uchaguzi wanavuruga mchakato huo ambapo wagombea wamekua wakitaliwa fomu zao.