Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka waagizaji wa magari nje ya nchi kutokuagiza magari kwa watu binafsi badala yake watumie Makampuni yanayoaminika na kufahamika ili kuepuka kupata hasara kama gari likiwa halina ubora wa viwango unaotakiwa.
Akizungumza leo akifungua mafunzo kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya majukumu ya Shirika hilo yaliyofanyika Makao Makuu ya TBS leo Jijini DSM Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Athuman Ngenya amesema kuwa uagizaji wa gari kupitia kampuni inayofahamika ni bora kwa maana tatizo lolote llinalohusu gari ambalo limegizwa kupitia kampuni hiyo itahusika.
“Kama ikitokea muagizaji wa gari atakuta kuna hitirafu ya gari basi kampuni aliyoitumia itahusika na matengenezo na kama muhusika hatatumia njia hiyo basi atakuwa kapata hasara kwani litakuwa limekosa viwango vinavyotakiwa” Dkt.Ngenya.
Aidha kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi Mhandisi Said Mkwawa akizungumzia kuhusu ukaguzi wa magari yatokayo nje ya nchi amesema ukaguzi huo pia umefanikisha kukusanya kiasi cha bilioni 1.5 ambazo hapo awali wangepata asilimia 30 pekee
“Katika magari 4779 tulioyafanyia ukaguzi kuanzia mwezi aprili 15 mpaka June 08, asilimia 85 ya changamoto kubwa imejitokeza kwenye ubovu wa kashata,taa, na magurudumu kuisha muda wake”. Mhandisi Mkwawa.
Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athumani Ngenya akifungua mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upimaji na Ugezi wa TBS, Mhandisi Johannes Maganga akizungumza katika hafla ya mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Maabara ya Kemia Bw.Charles Batakanwa akiwasilisha mada ya “Uwekaji wa Vinasaba katika Mafuta” katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje ya nchi, Mhandisi Said Mkwawa akiwasilisha mada ya “Ukaguzi wa Magari yaliyotumika yaliyowasili nchini ” katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Dar es Salaam. Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bw.Diocles Ntamulyango akidadavua jambo kwenye mada ya “Ukaguzi wa Magari yaliyotumika yaliyowasili” katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam .
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko Gladness Kaseka akiwasilisha mada ya “Majukumu ya TBS” katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari yaliyofanyika leo Makao Makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.