Top Stories

“UKIMWI mwisho 2030” Baraza Kuu UN

on

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kisiasa la kuyamaliza maradhi ya UKIMWI ifikapo mwaka 2030 ambapo Wanachama wa Baraza hilo kuu wameahidi kupunguza kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI hadi 370,000 na vifo vitokanavyo na UKIMWI hadi chini ya 250,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI, UNAIDS, Winnie Byanyima amesema bado Nchi nyingi hazijafikia ahadi zao na kuonya kuwa janga la COVID-19 linaweza kuibua upya janga la UKIMWI.

Tayari Mataifa wanachama yamekubaliana kulimaliza janga la UKIMWI kwa kuifikia asilimia 95 wa Watu wanaoishi na VVU dunaini, asilimia 95 ya usambazaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU na asilimia 95 ya Watu wenye virusi sugu dhidi ya dawa.

RAIS SAMIA NA KIKWETE MSIBANI KWA MZINDAKAYA, TAZAMA ALIVYOINGIA

Soma na hizi

Tupia Comments