Baada ya headlines nyingi kuandika juu ya uamuzi wa aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Canavaro kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa, baada ya kuvuliwa unahodha na kupewa Mbwana Samatta. January 20 Sports Extra ya Clouds FM iliongea na kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa.
Mkwasa aliongea na Sports Extra juu ya taarifa kumfikia kupitia vyombo vya habari ila yeye bado atambui uamuzi wa Canavaro kuhusu kujiondoa kwake, kwani bado yupo kwenye mipango yake. Mkwasa ameeleza kuwa hata kama Canavaro akiamua kustaafu rasmi, basi lazima waandae utaratibu maalum wa kumuaga kama nahodha mstaafu, ikiwemo kuandaa mechi maalum.
“Hili suala nafikiri sio vizuri kulizungumzia sana na nikizungumza nitazidi kulichochea, lakini maamuzi yatabaki kama yalivyokuwa, naheshimu maamuzi ya Canavaro kwani ni kiongozi mzuri muhamasishaji, ukweli nilimpa taarifa ila sitaki kulumbana, bado namuhitaji nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa amestaafu lakini mimi sitambui bado namuhitaji kikosini” >>> Mkwasa
Nadir Haroub Canavaro alitangaza kujiondoa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, baada ya kocha wake Boniface Mkwasa kumvua unahodha na kumpatia Mbwana Samatta, bila kupewa taarifa rasmi ya heshima. Canavaro anasema hachukizwi na Samatta kupewa unahodha ila ameumia kuona kuwa hajaheshimika, kwani taarifa za kuondolewa unahodha amepata kupitia vyombo vya habari.
Unaweza msikiliza Mkwasa hapa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.