Kutoka Johannesburg South Africa Mwimbaji Staa wa Bongofleva Ommy Dimpoz amezungumza kwa mara ya kwanza toka alipoanza kuumwa, kwenye sehemu ya kwanza ya mahojiano yake Ommy ameongea ukweli wa ugonjwa unaomsumbua na mengine.
- Namshkuru Mungu naendelea vizuri kwakweli, dua na dawa zimenisaidia…. maradhi huwa yanaanza taratibu lakini yangu ilivyoanza ilikua tofauti kidogo kuna siku tu nilishangaa nimeamka nikawa napata tabu kwenye kula, chakula wala maji havishuki.
- Nilikwenda Hospitali Tanzania nikaambiwa naumwa kansa, hiyo taarifa ya kansa ilinishtua sana na kunifanya niwaze sana lakini sikukata tamaa.
- Gavana Joh wa Mombasa alinisaidia sana kiukweli, aliwapigia simu Madokta wake wakasema twende Kenya kupimwa zaidi, Kenya ndio wakanipa vipimo vya kwanza vilivyonipa mwanga.
- Niliondoka Tanzania May 2018 na ndio sijarudi mpaka leo, Kenya nilianza vipimo upya na wakakata nyama kuangalia kama ni kansa kweli, majibu yaliyotoka yalikua na utata, wakakuta kuna vitu vingine ndani ambavyo walisema kwa vipimo vile kuna kipimo kingine kinahitajika lakini hakipo Kenya hivyo ni bora kwenda South Africa au India.
- Ommy Dimpoz ameiambia millardayo.com South Africa >>> “Wakati tukiwa Kenya Madaktari waliniuliza ‘umewahi kunywa sumu?’ wakaniambia kesi yako ina dalili zote kwamba ulikula au umekunywa kitu ambacho ni sumu, wakaniambia hiyo sio food poison bali ni sumu kabisa, majibu hayo yalinipa taharuki…. tukaja South Africa kuanza matibabu mara moja.
Sehemu ya kwanza ya EXCLUSIVE INTERVIEW na Ommy Dimpoz itapatikana kwenye YouTUBE ya millardayo na millardayo.com kuanzia leo usiku, sehemu ya pili itapatikana kesho.
ON AIR: ALIKIBA NA OMMY DIMPOZ WALIVYOULIZANA MASWALI