Bado imekuwa ngumu moja kwa moja Tanzania kufahamu kwa data kamili kati ya Yanga SC na Simba SC ni timu gani ina mashabiki wengi zaidi ya mwenzake, upande wa mashabiki wa Yanga wanaamini wao ndio wana mashabiki wengi zaidi ya Simba na Simba wanaamini hivyo hivyo wao wana mashabiki wengi zaidi ya Yanga.
Club za Simba na Yanga zimepishana mwaka mmoja tu kuanzishwa kwake, Yanga ikianzishwa mwaka 1935 na mwaka mmoja baadae ikaanzishwa Simba SC, hivi ndio vilabu vikongwe zaidi Tanzania, msemaji wa Simba Haji Manara kama kawaida yake leo amepost picha ya kuwakosoa wanaosema Yanga ndio club yenye mashabiki wengi zaidi.
“Siku hizi sisikii zile lugha za walevi eti Yanga ndio team ya Serikali au kujiita team ya Wananchi!!, Nchi yetu Serikali haina team na Wananchi ni Watanzania wote!!”
“Taasisi zote rasmi na kwa vigezo vyovyote vile zimethibitisha pasi na roho mbaya kuwa Simba ndio klabu inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi Tanzania”
“Anzia kwa kujaza viwanja kote nchini na hata dunia ya social media tumewacha maili milioni Gongowazi, Kiufupi haipo na haijaundwa any footboll club inayoweza kujaza umma huo kwenye friend match Afrika nzima, Kabla ya kunitolea povu nipinge kwa data”
“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe