Rais John Magufuli amewateua Majaji 6 wa Mahakama Kuu, kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakimu na Wanasheria 15 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.
Pia Rais Magufuli ameteua Wakuu wa Wilaya wawili ambapo amemteua Thomas Abson kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Charles Kabeho kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime.