Upande wa Serikali umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa bado inawatafuta Raia wanne wa Msumbiji na mmoja wa Afrika Kusini wanaodaiwa kumteka nyara mfanyabiashara Mohammed Dewji ( ‘MO’).
Mshitakiwa mmoja ambaye ni dereva tax na Mkazi wa Tegeta , Mousa Twaleb (46) tayari alishafikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Shaidi kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na wanaendelea kuwasaka washitakiwa wengine watano.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, 2019.