Serikali imelaani mauaji ya kinyama ya watoto watatu wa familia moja yaliyotokea Mkoani Njombe na kusema kuwa tukio hilo halitapita bure na inataka iwe fundisho kwa watu wengine wenye roho za kinyama wanaotekeleza mauaji ya watoto wadogo hapa nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni amelaani vikali tukio hilo wakati wa mazishi ya watoto watatu ndugu, Godliver, Giliad na Gasper Nziku ambao wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa maeneo tofauti Mkoani Njombe.
WATOTO WATATU NDUGU WACHINJWA NA KUNYOFOLEWA VIUNGO, ‘WALICHUKULIWA NA BAMDOGO’