Leo February 8, 2019 Nakusogezea stori kutoka nchini India ambapo Kijana Raphael Samwel mwenye umri wa miaka 27 amepanga kufungua kesi dhidi ya Baba na Mama yake mzazi kwa kumzaa bila idhini yake.
Raphael amesema anajua ni vigumu kwa Wazazi kuomba ruhusa kwa Mtoto kabla ya kumzaa. Anasema hakuna Mtoto aliyekubali kuzaliwa ili aje ateseke na maisha ya hapa duniani.
Wazazi wa kijana huyo ambao wote ni Wanasheria wamesema wanajisikia fahari kuwa na Mtoto kama yeye lakini wangetamani awaeleze ni namna gani wangewasiliana naye na kumhoji kama yuko tayari kuzaliwa nao.
WAKIMBIZI WAFURAHI KUMUONA ALIEMUOMBA RADHI RAIS MAGUFULI IKULU