Leo June 2, 2018 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa maafisa wa ngazi za juu ya serikali yake wanaohusishwa na ufisadi watapimwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kubaini watu waongo ili kukabiliana na ufisadi uliokithiri nchini humo.
“Kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyakazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo” Rais Kenyatta.
Rais Kenyatta alinena hayo baada ya kufichuliwa kwamba shilingi bilioni 8 za Kenya zilitumbuliwa katika idara moja ya serikali.
Kashfa hiyo ambayo imetokea katika shirika la vijana la huduma kwa jamii NYS ambapo vyeti bandia na malipo ya ziada yalifanyika wakati wahusika ambao ni wauzaji wa bidhaa waliokuwa wanatakiwa kulipwa hawakulipwa kama vyeti na hati za malipo hizo feki za zinavyoonyesha.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais Kenyatta alipokuwa akihutubia wananchi kwenye sherehe za miaka 55 tangu Kenya ipate uhuru ni kwamba, wakuu wote wa idara za kutoa zabuni na zile za serikali watafanyiwa ukaguzi mpya ikiwemo kupimwa na kifaa maalumu cha kuwabaini watu waongo ili kujua maadili yao.
“ Maafisa watakao feli watasimamishwa kazi” alisema rais Kenyatta.