Inaripotiwa kuwa Jay Z na Beyonce walivamiwa wakiwa kwenye stage wakiperform mjini Atlanta Marekani siku ya August 25,2018 katika ziara yao ya On The Run II (ORTII).
Uvamizi huo ulifanyika baada ya shabiki mmoja kupata nafasi ya kupenya na kufanikiwa kuwakwepa walinzi na kuamua kupanda jukwaani na kuanza kuwakimbilia Jay Z na Beyonce na ndipo wawili hao walilazimika kukimbia na kushindwa kuendelea na muziki.
Baada ya Beyonce na Jay Z kukimbia ndipo wachezaji waliacha kucheza na kutoa msaada huku wakionyesha ishara kuwa wamevamiwa, walinzi walifanikiwa kuwasaidia na kumkamata shabiki huyo na taarifa kuripoti kuwa wawili hao wapo salama na wataendelea na ziara yao kama kawaida.
Biashara anayoifanya Mzee wa zaidi ya miaka 80