Baada ya Diamond Platnumz kuzungumza kwenye press ya leo October 30, 2019 ya uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival DSM kuelezea kwamba Manager wake Babu Tale amewasiliana na Alikiba kuhusu kushiriki Wasafi Festival ya DSM.
Muda mfupi uliopita Alikiba ameandika kuwa – “Usiniletee mambo ya darasa la Pili unaniiibia penseli alafu unanisaidia kutafuta .(UNIKOME) Mwanaume huwa anaongeaga mara moja tu sasa ukitaka nikuweke uchi watu wajue unayonifanyia hata kwenye hilo tamasha hatokuja mtu sasa tuishie hapo nakutakia tamasha njema @diamondplatnumz”