Michezo

Wachezaji 10 wanaoongoza kwa kutoa pasi za magoli Ligi Kuu Uingereza msimu huu …

on

Kwa sasa Mesut Ozil hadi anaondoka ndani ya klabu ya Real Madrid ya Hispania na kujiunga na Arsenal ya Uingereza ndio alikuwa mchezaji anayeongoza kumpa pasi za mwisho Cristiano Ronaldo na kufunga magoli. Achana na rekodi ya sasa ya Mesut Ozil ya kuwa mchezaji anayeongoza kutoa pasi nyingi za magoli kwa muda mchache.

1

Hii ndio list inayoshikilia rekodi ya muda wote ya utoaji pasi za magoli (assist) katika Ligi Kuu Uingereza kwa msimu mmoja

Nimekutana na list ya wachezaji 10 wa Ligi Kuu Uingereza wanaoongoza kwa kutoa pasi za magoli katika msimu huu wa 2015/2016. Huenda zisiwe taarifa njema kwa mashabiki wa Man United na Chelsea ila ukweli hakuna mchezaji wao hata mmoja, pasi za mwisho za magoli alizopiga Ozil pekee yake msimu huu amezidi pasi za magoli za Chelsea kwa wachezaji wote na Manchester United pia.

cq5dam.thumbnail.490.338.margin

Hizi ni takwimu za kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ambaye anatajwa kushuka kwa umahiri wake wa utoaji pasi za magoli (assist) akiwa na Arsenal 2009/2010 alitoa pasi 13 na msimu 2014/2015 alitoa pasi 9.

Ozil amefanikiwa kupiga jumla ya pasi za magoli 15 katika michezo 16 msimu huu, wakati kikosi cha Chelsea kimepiga jumla ya pasi 11 za magoli msimu huu na Man United pasi 12 katika mechi 16 hizo ni jumla ya pasi za wachezaji wote. Mtu wangu wa nguvu ni halali yako kuipata hii, TOP 10 ya wachezaji wanaongoza kwa kupiga pasi za magoli msimu huu yaani assist (mchango wa mchezaji katika kusaidia ufungaji wa goli).

Capture30

Hii ndio list inayoongoza hadi sasa msimu huu kwa idadi ya mechi 16 za msimu huu pekee

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments