Najua nina watu wangu mnaotamani kufahamu historia ya wasanii pindi bado hawajajulikana katika tasnia ya sanaa ukiwa na amu ya kufahamu tabia au kitu alichokuwa analichokuwa anapenda msanii enzi za utoto wake.
Sasa basi ripota wa millardayo.com amekutana na Baba mzazi wa Mo Music Martin Katemi na kuzungumza naye kuhusu historia ya msanii Moshi aka Mo Music.
‘Mimi ni Martin Katemi baba mzazi wa Moshi nyie mnamfahamu kama Mo Music nina watoto wawili wa kiume yeye ni wa pili,kijana wangu enzi za utoto alikuwa anapenda sana kukaa na makundi ya vijana wenzake na kuna muda alikuwa anakuja nao marafiki zake nyumbani’ – Martin Katemi
‘Makundi yake walikuwa ni watu wa kutengeneza vitu kama magari pia hata ufugaji wa Mbwa ni mpenzi sana wa Mbwa kuna wakati alikuwa anajibishana sana na marafiki zake kuhusu ufugaji wa Mbwa na alipofikia darasa la saba alikuwa na kundi la muziki ambapo walikuwa wakienda mlimani hapa ulipo ukiangalia juu kuna eneo la mlima unaitwa Mlima wa Papa’ – Matin Katemi
‘Kule walikuwa wanafanya uimbaji lakini sisi wazee tulifanya kazi kubwa sana ya kuchuguza ni kitu gani wanachokifanya kwani kule ni eneo ambalo huwa wanakaa wahuni wavuta bangi na watu wengine lakini tulivyokwenda tukawakutana wana ma guitar na vifaa vya muziki baadae ndipo tukaanza kuona matunda kutoka kwa Mo Music baada ya kutoka wimbo wake wa kwanza’ – Martin Katemi
‘Na nyumbani kwao Mo Music ndio kando kando ya huo Mlima na ndio maana alikuwa akienda huko kwenda kufanya mazoezi yake na marafiki zake’ – Martin Katemi
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Baba wa Mo Music
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos