Maroc Export na BMCE Bank ya Afrika leo zimezindua kongamano la ‘African Business Connect 2017’ kwa upande wa Tanzania likiwa limehudhuriwa na zaidi ya washiriki 300 kutoka Tanzania na Morocco.
Dhumuni kuu la mkutano huo ni kuiwezesha Morocco kuunganisha uchumi wake katika uchumi wa Afrika pia kuunganisha fursa za biashara za Tanzania kwa kuibua maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi katika nyaja za umeme/nishati mbadala, uagizaji na usafirishaji wa bidhaa, ujenzi, usafiri, mawasiliano ya simu, fedha na mengine.
Kongamano pia lilitoa fursa ya kusaini mkataba wa makubaliano ya Ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Kituo cha Kuhamasisha Uwekezaji Morocco. Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk.Khalid Salum Mohammed. Unaweza kubonyeza hapa chini kuitazama
VIDEO: Mikataba 22 iliyosainiwa na Tanzania na Morocco, Bonyeza play hapa chini kuitazama