Wizara ya mambo ya nje ya Morocco imesema kwamba kuanzia Jumatatu itasitisha safari za ndege kuingia nchini humo kwa muda wa wiki mbili.
Hatua hiyo ni kutokana na aina mpya ya virusi vya corona vya Omicron. Kwa mijibu wa shirika la habari la AP, Wizara hiyo imesema kwamba hatua hiyo ni ya kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya janga hilo na kulinda afya za raia wake.
Taifa hilo hata hivyo ni miongoni mwa yale yaliyojitahidi kutoa chanjo kwa watu wake huku asilimia 66 tayari wakiwa wamepokea walau dozi moja.
Hatua ya kufungwa kwa safari za ndege pia imechukuliwa na mataifa mengine mengi kote ulimwenguni ikiwa kama hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo vipya ambavyo kwa mara ya kwanza vilitangazwa Afrika kusini.