Huu ni moto ambao umetokea asubuhi ya March 06 2014 saa 5 mtaa wa Majengo wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo nyumba iliteketea na furniture zake.
Jeshi la Polisi lilifika kwenye eneo la tukio na kutoa onyo kwa Wananchi waliojikusanya kwenye eneo la tukio ambao walikua hawajui athari za moto wa gesi.
Watu hao hawakutii amri hiyo zaidi ya kusogelea eneo la tukio ambapo saa moja baadaye gari la zimamoto lilifika likiwa limechelewa manake tayari nyumba ilikwisha ungua.
Sababu kubwa ya kuchelewa kwa gari ni umbali toka Halmashauri ya jiji la Mwanza ambao unasemekana ni umbali wa dakika 45.