Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anajulikana kwa majigambo, kujisifia lakini pia anapenda kitu kizuri kiwe kwake.
Kama utakua unakumbuka vizuri Mourinho ni kocha anayependa mfumo wa kujihami kwa lugha za mpira wanaita kupaki Bus yaani ni mfumo ambao timu inashambulia kwa kushtukiza na kujihami kwa kiasi kikubwa… Lakini cha kushangaza aliwahi kukutana na timu yenye tabia zaidi ya zake alilalamika.
Sasa basi Mourinho amerudi tena kwenye headlines, kwa kuanza kejeli zake tena kwa kusema kuwa timu pinzani zina jaribu kununua mataji. Mourinho ameyasema hayo kufuatia klabu vya Manchester United kufanya usajili mkubwa msimu huu, kwa wachezaji kama Matteo Darmian, Memphis Depay, Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin vivo hivyo kwa upande wa Man City na Klabu ya Liverpool ambao nao wamefanya usajili kwa kutumia fedha nyingi.
Licha ya kukiri kuwa hata mwaka 2003 mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich alikuwa ananunua mataji klabuni hapo baada ya kuanza kununua wachezaji kwa gharama ya juu, kauli ya Mourinho inatafsirika kama hapendezwi na usajili wanaofanya timu pinzani licha ya kuwa soka limebadilika wamiliki wananunua wachezaji kwa gharama za juu.
Nimekusogezea video ya sekunde 30 ya kauli za Mourinho
https://youtu.be/y8hqDSOUuQU
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.