Michuano ya Kombe la Mapinduzi January 6 iliendelea kama kawaida kwa mujibu wa ratiba January 6 itachezwa michezo miwili ya Kundi A. Mchezo mmoja tayari umemamlizika kati ya JKU dhidi ya Jamuhuri kutoka Pemba. Huu ulikuwa mchezo ambao JKU ilifanikiwa kupata ushindi wa jumla ya goli 3-0.
Jamuhuri ambao walifanikiwa kuidhibiti Simba katika mchezo wa kwanza na kufanikiwa kutoka sare ya goli 2-2, walishindwa kufua dafu mbele ya wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU). JKU walianza kupata goli la kwanza dakika ya 3 kupitia kwa Emanuel Martin, goli la pili lilifungwa na Nassoro Mataro dakika ya 35.
Wakati goli la mwisho la JKU lilitiwa nyavuni na Mohd Abdallah dakika ya 72. Kwa matokeo hayo URA ya Uganda ambayo itacheza na Simba saa 20:15 bado inaongoza kundi hilo kwa tofauti ya magoli ikiwa na point tatu. Wakati Jamuhuri itasubiri kucheza mechi yake ya mwisho ya Kundi A dhidi ya URA na Simba dhidi ya JKU.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE