Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) leo July 11, 2017 imekutana na Waandishi wa Habari na kuzungumzia kuhusu urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 ambapo wamegusia juu ya watu wanaowadhamini wanafunzi ili wapate mikopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema:>>>”Mtu anayemdhamini mtu kukopa ana wajibu mkubwa sana…ukimdhamini mtu kukopa una wajibu wa aina zifuatazo; moja ni, kuisaidia Bodi ya Mikopo kuwafahamisha anapopatikana mtu yule mara tu anapomaliza na anapofuatiliwa wakati wa kulipa.
“Una wajibu wa kuhakikisha kwamba yule uliyemdhamini anarejesha. Huwezi kumdhamini mtu halafu ukamuacha tu hujui kama anarejesha.” – Abdul-Razaq Badru.
GUMZO LA ESCROW: Waziri wa zamani wa Nishati na Madini William Ngeleja ametangaza kurudisha Fedha za ESCROW ambapo amezitaja sababu kuu 5…unaweza kuzifahamu kwa ku-PLAY hii VIDEO hapa chini!!!