Top Stories

Mshukiwa wa ugaidi ajilipua

on

Mshukiwa wa Ugaidi nchini Kenya ambaye Polisi wanadai alipewa mafunzo na Al Shabaab, John Odhiambo Ondiek amefariki baada ya kujilipua na bomu lililotengenezwa kienyeji ambalo limewaua pia Watu wengine wawili (Mke na Mume).

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kamloma Kaunti ya Kisumu usiku wa kuamkia leo ambapo Mlipuaji huyo alienda hadi nyumbani kwa Petro Onyango (54) akamkuta akiwa amekaa na Mkewe Mary Atieno (40) na Mtoto wao Nancy Aoko (14) na akaanza kuwauliza mambo ambayo hawayakuyaelewa na ghafla akajilipua mabomu ya asili ambayo aliyavaa kiunoni na yeye pamoja na Mary wakafariki papohapo.

Petro Onyango alifariki njiani akipelekwa Hospitali na Mtoto wao Nancy bado anaendelea kutibiwa Hospitalini baada ya kupata majeraha.

Polisi wanasema baada ya kuuona mwili wa Odhiambo wamebaini kuwa aliwahi kutaka kumuua Mkewe December 17,2020 kwa kumlipua na bomu akimtuhumu kuwa anamsaliti lakini alifanikiwa kukimbia na tangu siku huyo Mke huyo hajaonekana tena hadi leo.

EXCLUSIVE: FUNDI ALIYENUSURIKA KIFO GOROFA LA GOBA ASIMULIA “LILISHUKA GHAFLA WAAAH, NIKARUSHWA”

Soma na hizi

Tupia Comments