Timu ya taifa ya Ufaransa usiku wa July 15 2018 katika uwanja wa taifa wa Urusi unaojulikana kwa jina la Luzhniki wameweka historia mpya baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Kombe la Dunia kwa mara pili katika historia toka watwae taji hilo kwa mara ya kwanza 1998.
Ufaransa wametwaa taji la World Cup 2018 kwa kuifunga Croatia kwa jumla ya magoli 4-2,magoli ya Ufaransa yalipatikana kwa Mario Mandzukic kujifunga dakika ya 19, Antoine Griezmann kwa mkwaju wa penati dakika ya 38, Paul Pogba dakika ya 59 na Kylian Mbappe dakika ya 65 huku ya Croatia yakifungwa na Ivan Perisic dakika ya 28 na Mario Mandzukic dakika ya 69.
Croatia ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo katika historia, huku wakiweka rekodi ya kuwa taifa dogo lenye watu milioni 4.5 kuwahi kufika fainali ya World Cup, inawezekana ukawa ufahamu baadhi ya mambo kutoka katika kikosi cha Ufaransa.
Michuani ya World Cup 2018 kila taifa lilipewa nafasi ya kuita wachezaji 23 itakaowatumia katika michuano hiyo ya fainali za Kombe la Dunia ila kuna hii ya Ufaransa inawezekana ukawa hauifahamu, zaidi ya asilimia 80 ya wachezaji wa Ufaransa walioshiriki World Cup 2018 hawana asili ya Ufaransa.
List ya wachezaji 23 wa Ufaransa walioitwa kulitumikia taifa hilo na kutwaa Ubingwa wa World Cup ni wachezaji watano pekee ndio wanaasili ya Ufaransa, huku 15 wakiwa wana asili ya Afrika na wachezaji watatu waliosalia wakiwa na asili ya mataifa ya Italia, Ujerumani, Ureno na Hispania.
Hii ni list ya wachezaji 15 wenye asili ya Afrika na wameichezea Ufaransa World Cup 2018.
1- Presnel Kimpembe baba yake anatokea Congo
2- Samuel Umtiti amezaliwa Cameroon
3- Paul Pogba wazazi wake wote wawili wanaasili ya Guinea
4- Kylian Mbappe baba yake anatokea Cameroon na mama yake Algeria
5- Ousmane Dembele mama yake ni Mauritania mwenye asili ya Senegal
6- Corentin Tolisso alikuwa na nafasi ya kuichezea Togo kutokana na asili ya familia yake 2015 aliitwa timu ya taifa ya Togo na kugoma kwenda kuitumikia akachagua Ufaransa.
7- N’golo Kante wazazi wake wanatokea Mali
8- Blaise Matuidi baba yake anatokea Angola na mama yake Congo
9- Steven N’zonzi ana asili ya Congo DRC
10–Steve Mandanda amezaliwa Congo DRC
11– Nabil Fekir wazazi wake wana asili ya Algeria
12- Djibril Sidibe anahusishwa kuwa na asili ya Mali
13- Benjamin Mendy wazazi wake wana asili ya Senegal
14- Thomas Lemar ana asili ya Nigeria na Guadeloupe
15- Adil Rami wazazi wake wana asili ya Morocco
List ya wenye asili ya mataifa mengine Ulaya
1- Olivier Giroud ana asili ya Italia upande wa bibi yake
2- Antoine Griezmann ana asili ya Ujerumani na Ureno upande wa mama
3- Lucas Hernandez baba yake ana asili ya Hispania
LIST YA WALIO NA ASILI YA UFARANSA
1- Raphael Varane
2- Benjamin Pavard
3- Hugo Lloris
4- Alphonse Areola
5- Florian Thauvin
Mashabiki wa soka Escape One wakishuhudia Ufaransa ikitwaa Ubingwa World Cup