Deothilla Makayula ni Mwanamke wa Kitanzania ambaye aliamua kuachana na kazi na kujiingiza kwenye ujasiriamali ambao anakiri umempatia faida kubwa na kumfanya apate muda mwingi wa kukaa na familia yake, wakati huu ambapo jitihada mbalimbali zinafanywa Duniani kote ili kupambana na corona, Deothila hajabaki nyuma na yeye ameamua kujitosa kwenye mapambano.
“Nilipitia mengi nilikatishwa tamaa, nilianza biashara baada ya kupata matatizo ya kiafya hasa katika mlango wa kizazi, licha ya kuwa hakuna dawa wala chanjo ya corona, nimekuwa nkiifundisha jamii kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kutumia chakula lishe na namna bora ya kuongeza kinga mwili”– Deothilla
CORONA TANZANIA: VISA VYAFIKIA 306 “WAMEPONA WAGONJWA 84”