Baraza la Mitahani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya Watahiniwa 540 wa vituo sita (06) ambavyo ni Joyland (PS0206131), Castle Hill (PS0204150), Green Acres (PS0203129), Great Vision (PS0206099), Mtendeni (PS0202026) na Maktaba (PS0202058) vote ya mkoa wa Dar es Salaam ambao wanatuhumiwa kufanya udanganyifu mpaka uchunguzi utakapokamilika.
“Wakibainika kufanya udanganyifu matokeo yao yatafutwa kwa mujibu wa Kifungu Na. 4(8) cha Kanuni za Mitihani 2016 na endapo
hawatabainika kufanya udanganyifu watapewa matokeo yao”
Baraza la Mitihani pia limezuia kutoa matokeo ya Watahiniwa 179 ambao waliugua/walipata matatizo na kushindwa kufanya mtihani kwa
masomo yote au baadhi ya masomo.
“Watahiniwa husika wamepewa fursa nyingine ya kurudia kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2023 kwa mujibu wa kifungu 32 (1) cha Kanuni za Mitihani”