Zikiwa siku chache tangu kesi yake ianzwe kusikilizwa kwenye mahakama ya wilaya ya Ilala Dar es salaam Emmanuel Mbasha ambaye ni mume wa mwimbaji wa nyimbo za injili Flora Mbasha,baadhi ya wadau wametoa ya moyoni juu ya kesi hii.
Miongoni mwa watu walioguswa na kutoa ya moyoni ni muongozaji wa filamu mbalimbali Tanzania Wiliam Mtitu ambaye katika ukurasa wake wa Instagram alipost picha ya Flora Mbasha akiwa na Mumewe Emanuel Mbasha kisha kuandika maneno haya chini ya picha hiyo.
‘Ukiiangalia vizuli hii picha utagundua kitu katika macho ya frola mbasha kuna kitu nakiona kinejificha lakini sasa hivi kimeshajitokeza tayali…..hicho kitu ndicho kilichompeleka jera mbasha na asipokuwa makini anaweza asiwe uraiani tena kama ulivyowatokea familia ya nguza .namaanisha mzee nguza na papii kocha wako wapi? Kiukweli frola una roho mbaya ya mwisho kabisa ilichanganyika na ukatili wa mwisho kabisa kiasi kwamba nashindwa kuelewa umeokoka nn ww ? Eti umemrudia YESU ?YESU yupi huyu nnaemwabudu mm au una YESU wako ww na HUYO GWAJIMA wako? Leo umemsahau Mbasha ww ? Wakati alikuokata umechakaa wakati mbasha dereva teksi leo wataka kumfunga ili iwe nn sasa mbasha akifungwa utapata faida gani ww? Huyo mtoto akija kukuuliza baba yuko wapi utamwambiaje? Fine unaweza kujikaza ukamwambia yuko jera je akikuuliza nani alimshitaki utajibu nn ? Pia waweza kujikaza ukawataja hao wasichana mliowapandikiza je akiuliza ww ulifanya jitihada gani baba asifungwe utasemaje? Hapo auna jibu Acha roho mbaya NENDA KAMTOE MARA MOJA NA MWENDE NYUMBANI MKAONGEE KAMA FAMILIA TWAJUA UWEZO HUO UNAO ILI NA YEYE ATAFUTE HAMSINI ZAKE KAMA WW ULIVYOAMUA KUJISALIMISHA KWA GWAJIMA. USIJE UKASHANGAA WATU WAKASUSIA KAZI ZAKO ZOTE. GDAY.
Hata hivyo upande wa Jamhuri ulitoa hoja ya kuwa hauna pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa,Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshitakiwa ambayo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili.
Mmoja kati ya wadhamini hao awe ni mfanyakazi wa serikali,mwingine atoke kwenye taasisi inayotambulika,wote kama wapo,walitakiwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 5 kwa kila mmoja.
Mbasha alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo hakimu aliamuru apelekwe kwenye Mahabusu ya Keko jijini Dar ambako atakuwa chini ya ulinzi,ingawa inasemekana kuwa leo June 19 anategemewa kurudishwa tena mahakamni.