AyoTV

VIDEO: Mama wa mtoto mwenye kipaji asema kwa Bukoba hajaona shule ya kumpeleka

on

Mtu wangu inawezekana ulikutana nacho kipande cha video ambacho kilianza kwa kusambaa mtandaoni kikimuonyesha mtoto ambaye ana uwezo wa kuwataja viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi sasa wazazi wa mtoto huyo wameeleza kwamba sababu ya mtoto huyo kuwajua viongozi ni kwa sababu amekuwa na tabia ya kufuatilia taarifa za habari na akimaliza ataanza kuuliza maswali wazazi wake.

Wazazi wake wamesema imepita miezi minne tangu wagundue uwezo wake huo wa kukariri aidha wazazi wamesema akifundishwa inamchukua kama dakika 10 anakuwa ameshakariri.

Kwenye video hii hapa chini mama wa mtoto huyo ameeleza mpango wa kumpeleka shule ambapo amesema………>>>‘tunataka mwezi wa kwanza ndio tumpeleke shule, tumtafutie shule ambayo itamfaa maana kwa Bukoba hii sijaona’

ULIKOSA WALICHOKIONGEA WAZAZI WA MTOTO MWENYE KIPAJI CHA KUWATAJA VIONGOZI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments