Mwezi uliopita Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya wabunge wa vyama vya upinzani kumzomea wakati akitoa hotuba wakimshutumu kushindwa kuiongoza vyema nchi yao.
Headlines zimerudi tena kwa Rais huyo baada ya jana Bunge hilo kuahirisha matangazo ya LIVE ya redio na Televisheni ya hotuba ya Mugabe kutoka kwa vyama vya upinzania wakitishia kuvuruga hotuba hiyo kwa mara nyingine.
Wapinzani hao wamekua wakimlaumu rais wao kuendelea kung’ang’ania madarakani wakati uchumi wa nchi hiyo ukizidi kudidimia kila siku.
Rais Mugabe ambaye sasa ametimiza miaka 91 amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.
Spika wa Bunge Jacob Mudenda amevionya vyama hivyo kuacha mara moja vurugu hizo lakini juhudi zake ziligonga mwamba na kusababisha vituo vya matangazo kusitisha kurusha matangazo hayo LIVE.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos