Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linawashikilia watu wawili akiwemo aliechukua mke wa mtu na aliechukuliwa mke wake na kujichukulia hatua mikononi mwake baada ya kumfumania mke wake na Mwanaume mwingine aliefahamika kwa majina ya Mundhir Khamis Karama (32)
Mundhir anadaiwa kumchukua mwanamke na kumpeleka nyumbani kwake huko Kijichi. Baada ya muda mfupi wakiwa chumbani alivamiwa na watu watano ambao mmoja wao alidai kuwa mume wa mwanamke huyo.
Watu hao walimshambulia kwa fimbo na vitu vyenye ncha kali kisha kumfunga kitambaa usoni na kuondoka nae kusikojulikana kwa gari aina ya Noah na watu hao walimpora Mundhir simu aina ya Samsung yenye thamani ya Tsh.400,000 pamoja na kisha kumtaka apige simu kwa ndugu zake ili watume pesa ndipo aachiwe
Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa walioshiriki katika tukio hilo ambao ni Khamis Seif Khamis, me (30) na mke wake (Aliekutwa ndani ya chumba na Mundhir).
Aidha juhudi za kuwakamata watuhumiwa wengine zinaendelea
Tazama zaidi…