Leo tunakupitisha ujionee maendeleo ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange), mradi huu wa ujenzi katika Makutano ya Barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma unaendelea kwa kasi kubwa, March mwaka huu ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 70.
Mradi huu utakamilika kwa gharama ya Tsh.Billion 230 na unatarajiwa kuondoa adha ya msongamano mkubwa katika makutano ya barabara hizi pindi utakapokamilika.