Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Jopo la Majaji watatu imesikiliza maombi ya rufaa ya Serikali ya Tanzania ya kupinga uamuzi wa kubatilishwa kwa sheria ya ndoa za watoto walio chini ya umri wa miaka 18.
Katika uamuzi wa Awali Mahakama hiyo iliamua kuwa sehemu za sheria ya ndoa ya mwaka 1971, inayoruhusu wasichana kuolewa wakiwa na umri wa hata miaka 14 ni kinyume na katiba.
Katika usikilizwaji wa rufaa hiyo, Mahakama Kuu inatarajia kupanga tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi kama ikubaliane na hoja za Serikali kutetea sheria hiyo ama kuitupilia mbali.
JEBRA KAMBOLE AFUNGUKA KESI YA NDOA ZA UTOTONI “SERIKALI WANAITAKA”