Serikali imetumia takribani Bilioni 6 kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya maji taka maeneo ya Bwawani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na mafuriko hasa kipindi hiki cha mvua.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo amesema eneo hilo lina tabaka la maji ambapo baada ya mvua kuanza kukaibuka changamoto katika eneo hilo.
“Huu mradi ni wa gharama kubwa unatumia zaidi ya Bilioni 6 za serikali ya Tanzania na zimeletwa katika mtaa mmoja wa Bwawani kwa ajili ya kurekebisha miundombinu na kuweka mazingira safi ya eneo hili,“amesema.