Wakati mvua zikiendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Geita , baadhi ya nyumba pamoja na Kanisa la AIC lililopo Wilayani Chato Mkoani Geita yameezuliwa na mvua kubwa zilizokuwa zimeambatana na upepo mkali huku watu 4 ambao ni waumini wa kanisa hilo wakijeruhiwa hali ambayo imepelekea waumini kusalia nje.
Wakizungumza na AyoTV ilipowatembelea Wananchi hao wa Kata ya Minkonto Chato kijiji cha Minkonto baadhi ya waumini pamoja na wananchi wa eneo hilo wamesema mvua hizo zimeanza juzi majira ya Saa 11 za jioni na kusababisha hasara ya kiasi cha shilingi Milioni 10.
“Sisi tulikuwa ndani tulikuwa tuna sali ghafla tukasikia mvua inanyesha huku imeambatana na upepo mkali mda huo tupo kwenye kanisa tukawa tunapiga mziki tukasikia radi tukazima mziki baada ya hapo tukasikia kanisa linadondoka mda huo tumo ndani tunaomba serikali itusaidie, “ Waumini.
Benjamin Matumbati ni Mwenyekiti wa kanisa la AIC kata ya Minkoto Chato amesema wamehudhunishwa na tukio hilo huku wakiiomba serikali kuwasadia kutokana na athari zilizojitokeza wakati wkijiandaa ibada ya kuamkia Jumapili.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha Minkoto Chato Lipuli Stephano amesema tukio hilo la Mvua kubwa ambazo ziliambatana na upepo mkali zimesababisha athari kubwa katika kijiji hicho cha Minkonto pamoja na waumini wa kanisa la AIC Chato kuezuliwa huku wananchi 4 wakijeruhiwa mpk sasa wanaendelea na Matibabu.