Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imemkamata Mwalimu wa Shule ya Sekondari Embarway William Sambweti Mollel katika hoteli Mkoani Arusha akiwa na Mwanafunzi wa miaka 17 akiwa katika maandalizi ya kufanya nae ngono.
Kamanda wa TAKUKURU Arusha Frida Wikesy amesema Mwalimu huyo alikuwa akimpa manyanyaso Mwanafunzi huyo kwa lengo la kumtaka kingono ndipo walipoweka mtego na kumkamata.