Bado mjadala kuhusu kauli ya Mbunge wa Kenya Charles Kanyi maaarufu kama Jaguar kuhusu kuwapiga na kuwafukuza Raia wa kigeni wanaofanya biashara Kenya wakiwemo Watanzania, Waganda na Wachina upo kwenye vichwa vya habari ambapo Mastaa mbalimbali wa Tanzania wamesimama kupaza sauti zao.
Msanii MwanaFA ameandika yafuatayo baada ya Jaguar kuandika kwamba kauli yake imetafsiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa >>> “My brother @jaguarkenyaipo hekima kwenye kugundua ulikosea na kuomba radhi,uliteleza tu..apologize and lets move on,kila mtu hukosea..hii ya kuzunguka zunguka na maneno haitasaidia,haitaondoa hii kitu.. How did we misinterpret “tutawapiga”