Ni Mwanajeshi mwenye asili ya Tanzania anaelitumikia Jeshi la Marekani aitwae David.
David ameonekana mara kwa mara akiziimba nyimbo za wakongwe wa Zamani akiwemo Juma Nature na nyinginezo.
Mwanajeshi huyo mwenye asili ya Tanzania akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM aliwaomba Watanzania wathamini Muziki wa Wakongwe.
Nikimnukuu David anasema…’Napambana kutangaza lugha ya Kiswahili Marekani, Bongo Fleva inatufariji vitani, wengine hawanielewi wananiuliza hapa maana yake nini nawaelewesha, Muziki wa zamani bado naupenda sana hata washikaji zangu ninaofanya nao kazi katika hali ngumu ya baridi lakini tunapousikika unatufariji’
Ayo TV & Millardayo.com imekusogezea ufahamu alichozungumza Mwanajeshi wa Marekani mwenye asili ya Tanzania tusiyoyajua.