Lilian Lema ni mwanamke anayeishi Arusha ambaye amefanya kazi ya udereva kwa miak 17, lakini amepitia sehemu mbalimbali nakufanya kazi ikiwemo kazi ya kilimo na baadaye alibadilisha muelekeo nakwenda chuo cha VETA kusomea udereva na sasa hivi ameaminiwa nakuajiriwa kumwendesha mkurugenzi mkuu wa taasisi inayohusika na kuhudumia wakulima wa mbogamboga,matunda na maua TAHA
“hata wanaume wenyewe wananishangaa,askari wenyewe wanakuuliza mwanamke kama wewe unapitaje huku muda huu,na siogopagi kupita popote kwa wakati wowote kwa sababu namuamini Mungu na kazi zangu nyingi ni za usiku, kitu chochote ni malengo nakujiamini namshukuru Mungu nina boss mwanamke ambaye ana utu”-Liliani