Mkuu wa mkoa mstaafu wa Tabora Aggrey Mwanri amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu wa mkoa mpya Dkt. Philemon Sengati huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Tabora kushirikiana na kiongozi huyo ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo kama ilivyo adhma ya serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwanri amemshukuru Rais wa jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo kwa kipindi chote ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora.